Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 8:39 pm

TCRA: MPAKA SASA NI LAINI MIL 5.2 TU ZILIZOSAJILIWA KATI YA MIL 44.2

Dar es Salaam. Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kuwa mpka sasa ni laini za simu milioni 5.2 ndio zimesajili kwa alama za vidole kati ya watumiaji wasimu milioni 44.2 huku kukiwa kumesalia miezi mitatu tu kabla ya kukamilika kwa usajili huo ambapo Idadi hiyo ni sawa na asilimia 12% tu ya laini zote za simu zinazotumika hapa nchini Tanzania.

Tokeo la picha la usajili alama za vidole

Kwasababu ya kutokuwa na muitikio mkubwa wa usajili, watoa huduma wa mawasiliano nchini wa TCRA wameanzisha kampeni ya uhamasishaji inayolenga kuwahamasisha watumiaji wa simu kusajili laini zao. Kampeni hiyo inayoratibiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imezinduliwa leo Alhamisi Septemba 19, 2019 kwa kuzihusisha kampuni zote za simu nchini.

Tokeo la picha la usajili alama za vidole

Akizungumza leo mkuu wa kitengo cha mawasiliano kwa umma wa TCRA, Frederick Ntobi amesema hadi Agosti, 2019 laini milioni 5.2 ndio zimesajiliwa kati ya milioni 44.2. “Tunasisitiza baada ya Desemba 31, 2019 laini zote zitakazokuwa hazijasajiliwa kwa alama za vidole hazitaruhusiwa kutumika kwenye mitandao ya simu,” amesema Ntobi.

Akizungumza kwa niaba ya mwenyekiti wa watoa huduma za mawasiliano ya simu, mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa Vodacom Tanzania PLC, Alex Bitekeye amesema wameamua kushirikiana ili kuhakikisha wateja wanasajiliwa kwa wakati.

“Watoa huduma ni jukumu letu kuhakikisha laini zote zinasajiliwa, tumeona kuna uzito kidogo ndio maana tumeamua kushirikiana kufanya kampeni ya kuhamasisha,” amesema Bitekeye.