- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
TAKUKURU YATOA ONYO WATAKAOTOA RUSHWA UCHAGUZI SEREKALI ZA MITAA
Dar es Salaam. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imetoa onyo kali kwa watakaojihusisha na vitendo vya rushwa wakati wa zoezi la uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24, 2019.
Imesema Moja kati ya makosa yatakayowatia hatiani wagombea katika uchaguzi huo ni kugawa zawadi kwa wapiga kura Kama vile Jezi ya chama kwa ajili ya ushawishi.
Kauli hiyo imetolewa leo Jumamosi Septemba 21, 2019 na kaimu mkurugenzi mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo wakati akizungumza na waandishi wa Habari huku akisema miongoni mwa makosa ya rushwa wakati wa uchaguzi ni mpiga kura kupewa hongo ili asijiandikishe katika daftari la wapiga kura na kutopiga kura.
Amesema makosa mengine ni mgombea kujitoa kwenye kinyang’anyiro kwa sababu ya kuhongwa, kuamriwa mtu wa kumpigia kura na kutumia njia za rushwa kuandaa kundi la watu kufanya vurugu kwenye mikutano ya kampeni ili mgombea mwingine asipate fursa ya kujinadi vizuri kwa wapiga kura.
“Wanaotarajia kupiga kura hawapaswi kupokea fulana au kitu chochote ambacho kitahamisha utashi wake wa kumchagua kiongozi anayemtaka, zawadi yoyote yenye lengo hilo iwe, soda, chakula au kusafirishwa ni rushwa,” amesema Mbungo.
Hata hivyo, amesema vyama vina utaratibu wake wa kuvaa sare ambao huwezi kuingiliwa lakini kama sare hizo zitatolewa kwa lengo la kushawishi kupigiwa kura hiyo ni rushwa kwa kuwa ina athiri dhamira halisi ya mtu.
“Kujua kama mtu amepewa ‘tisheti’ kama rushwa hilo ni jambo gumu kidogo. Tunawasihi wananchi kuwa tayari kufichua wale wote watakaojihusisha na vitendo vya rushwa kabla, wakati na baada ya uchaguzi ikiwa ni pamoja na kuwa tayari kutoa ushahidi wa katika kesi zinazochunguzwa katika mapambano dhidi ya rushwa ,” amesema Mbungo.