- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
TAKUKURU YAMNASA KIGOGO SEREKALINI KWA KUOMBA RUSHWA YA MIL 12
Kagera: Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU), mkoani Kagera, inakusudia kumfikisha mahakamani kaimu meneja mkuu wa kampuni ya ranchi za taifa (NARCO) Prof. Philemon Wambura, kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa ya shilingi milioni 12, kutoka kwa mfanyabiashara mmoja aliyetaka kumpatia kitalu cha ufugaji Mkoani humo.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo Octoba 30, 2019, Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Kagera John Joseph, amesema kuwa mnamo Septemba 23 mwaka huu walipata taarifa ya Wambura kujihusisha na vitendo vya kuomba rushwa.
Aliomba rushwa kutoka kwa baadhi ya wafugaji wenye uhitaji wa vitalu vya kufugia ng’ombe, au wenye vitalu ambao wanahitaji kuhuisha mikataba yao ya awali.
Aidha mkuu huyo wa TAKUKURU amesema kuwa wamewafikisha mahakamani watu wengine wanne ambao wanakabiliwa na mashtaka ya kuomba na kupokea rushwa.