- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
TAARIFA ZA KIFO CHA MUIGIZAJI WA MOVE ZA JAMES BOND
Uswisi: Muigizaji maarufu wa move Duniani Roger Moore ambae ni nyota wa filamu alieigiza kwenye move nyingi kama James Bond, amefariki nchini Uswisi kwa ugomjwa wa Saratani akiwa na miaka 89.
Roger George Moore alizaliwa Oktoba 14, 1927 jijini London akiwa mtoto pekee wa afisa wa polisi mwenye cheo cha constable na mke wake, na alikulia katika maisha mazuri. Moore alianza kazi ya uingizaji kama msaidizi katika miaka ya 1940 kabla ya kusoma katika chuo cha kifalme cha masomo ya sanaa ya maigizo. Alipata mkataba wa studio za MGM lakini alikuwa tu na jukumu la usaidizi katika miaka 1950. Ilikuwa ni katik muongo uliofuata ambapo alipata umaarufu duniani, akiigiza katika kipindi cha televisheni cha Uingereza "The Saint" kama Simon Templer, mpenda vituko
Moore aliigiza kwa mara ya kwanza katika filamu ya "Live and Let Live", baada ya watengenezaji filamu kumwambia apunguze uzito, ili kuwa fiti na kukata nywele zake. Ambapo aliigiza filamu kama "The Man With the Golden Gun" (1974), "The Spy Who Loved Me" (1977), "Moonraker" (1979), "For Your Eyes Only" (1981) na "Octopussy" (1983) kabla ya kutupa daruga baada ya kuigiza "A View to a Kill" mwaka 1985, akiwa na umri wa miaka 57.