- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORTS: ZIDANE "NALAZAIMIKA KUMTEGEA GARETH BALE KWASASA"
Meneja wa miamba ya soka barani Ulaya Real Madrid Zinedine Zidane amesema kwa sasa "analazimika kumtegemea" mshambuliaji Gareth Bale licha ya kauli alizozitoa awali kwamba nyota huyo wa kimataifa wa Wales huenda akahama klabu hiyo msimu huu.
Kauli hiyo ya Zidane imekuja mara baada ya Kiongo wao pendwa aliyesajiwa kutoka club ya Chelsea Eden Hazard kuumia paja siku ya Ijumaa akiwa mazoezini sasa Bale huenda akategemewa katika mechi ya ufunguzi wa La Liga dhidi ya Celta Vigo Jumamosi ya leo.
Bale alitarajiwa kujiunga na klabu ya Jiangsu Suning inayoshiriki Super League ya Uchina mwezi Julai.
"Ilionekana kama ataondoka lakini kwa kuwa hakufanya hivyo nitamtegemea sawa na wachezaji wengine katika kikosi," alisema Zidane.
"Ana mkataba, na ni mchezaji muhimu, na kila mchezaji ananipatia wakati mgumu kuamua nani ajumuishwe katika kikosi cha kwanza au la."
Hazard, anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa kati ya wiki tatu mpaka nne, huku Real ikiendelea kumudu bila uwepo wa muda mrefu wa Marco Asensio na beki wa kushoto Ferland Mendy ambaye anauguza jeraha.
Majeruhi hayo yanamaanisha mchezaji nyota wa Colombia James Rodriguez pia ana nafasi ya kuiwakilisha klabu hiyo katika mashindano ya msimu huu baada ya kuwa na Bayern Munich kwa mkopo wa miaka miwili.
"Yuko sawa, na ni vyema amerudi," aliongeza Zidane.
Bale mwenye miaka 30 alijiunga na miamba hiyo ya Uhispania kwa dau lililovunja rekodi la £85m kutoka Tottenham 2013. Amesalia na kandarasi ya miaka mitatu katika uwanja wa Bernabeu ambapo ameshinda mataji manne ya ligi ya mabingwa Ulaya , taji moja la la Liga, mataji matatu ya Uefa na mataji matatu ya klabu bora duniani.