- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORTS: ZAHERA ASEMA HAIOGOPI TIMU YEYOTE
Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amejigamba kuwa, kikosi chake kipo tayari kumkabili mpinzani yeyote yule watakaye pangiwa naye na kumshida
Kauli hii inakuaja WAKATI wakisubiri droo ya mechi za mtoano ya kusaka tiketi ya kutinga hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika imepangwa kuchezeshwa leo.
Yanga iliangukia hatua hiyo, baada ya kutolewa Ligi ya Mabingwa Afrika na Zesco United ya Zambia, kwa kuchapwa jumla ya mabao 3-2, katika michezo miwili ya nyumbani na ugenini ya raundi ya kwanza.
Ilianza kulazimishwa sare ya bao 1-1 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam , kabla ya kukubali kichapo cha bao 2-1, katika mchezo wa marudiano uliochezwa Ndola, Zambia.
Baada ya kutupwa Shirikisho, vijana hao wa Jangwani wataanzia hatua ya mtoano, wakianzia nyumbani, ambapo mchezo wa kwanza utapigwa Oktoba 27, mwaka huu Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, kabla ya marudiano kuchezwa Novemba 3, mwaka huu.
Shirikisho la Soka Barani Afrika (Caf), limefanya mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa michuano hiyo, ambapo sasa timu zinazotolewa raundi ya kwanza ya Ligi Mabingwa Afrika hutua hatua ya mtoano ya Kombe la Shirikisho na huko hucheza michezo miwili ya nyumbani na ugenini.
Timu hizo 16 zilizofurushwa Ligi ya Mabingwa, huwekwa kapu moja na nyingine 16 zilizofuzu raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho, ili kuwania kufuzu hatua ya makundi.
Droo hiyo itakuwa ya wazi kwa maana, timu zote 32 zitawekwa chungu kimoja ili kusaka 16 zitakazounda makundi ya manne.
Orodha kamili ya timu zilidondokea Shirikisho zikitoka Ligi ya Mabingwa ni Yanga, Horoya (Guinea), Enyimba (Nigeria), Gor Mahia (Kenya) ,KCCA (Uganda), Asante Kotoko (Ghana), UD Songo (Msumbiji), Elect –Sport (Chad), Cano Sport Guinea ya Ikweta na Al Nasir ya Libya.
Nyingine ni Fosa Juniors (Madagascar), FC Nouadhibou (Mauritania), Côte d’Or FC (Shelisheli), ASC Kara (Togo) na Green Eagles ya Zambia.
Zilizofika hatua hiyo baada ya mapambano tangu raundi ya awali ni RS Berkane (Morocco), Al Masry (Misri,) Hassania Agadir (Morocco), Zanaco (Zambia), Enugu Rangers(Nigeria) na Djoliba Athletic Club ya Mali.
#Mtanzania