- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORTS: WAZIRI MWAKYEMBE AAHIDI KUMPA SAMATTA UBALOZI MAALUMU
Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Dkt. Harrison Mwakyembe, amefurahishwa na Mwenendo na mafanikio ya nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania na Mshambuliaji wa Club ya KRC Genk Mbwana Ally Samatta baada ya kuisaidia timu yake hiyo kuibuka mabingwa wa Ubelgiji kwa msimu wa mwaka 2018/2019.
''Samatta amefanikiwa kuipeperusha vizuri bendera ya Tanzania, ni shujaa ambaye mchango wake ni mkubwa na tunajaribu kuona ni vipi Samatta anaweza kuwa Balozi wa vivutio vyetu vya utalii, Sanaa na Michezo'', amesema Waziri Mwakyembe
Waziri Mwakyembe ametoa pongezi hizo mara baada ya Mtanzania kuwa kinara wa mabao kwenye ligi kuu ya Ubelgiji akiwa amefunga magoli 20 na kufanikisha kuisaidia club yake kubeba taji la ligi kuu.
Samatta alijiunga na Genk mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ambapo mwaka huo pia alishinda tuzo ya mchezaji bora wa ndani Afrika baada ya kufanya vizuri kwenye Ligi ya Mabingwa.
Mbwana Samatta ambeye ni mchezaji wa zamani wa Simba, TP Mazembe na mfungaji bora wa Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2016,