- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORTS: UEFA YATOA KIKOSI BORA CHA MWAKA, HAKUNA MWIINGEREZA HATA MMOJA
Timu ya taifa ya Uingereza imeshindwa kuingiza hata mchezaji mmoja kwenye wachezaji wanaounda kikosi bora cha mwaka 2018 kwenye Mashindano ya UEFA licha ya taifa hilo kufika hatua ya Nusu fainali kwenye mashindano ya Kombe la Dunia yaliyofanyika nchini Urusi.
Ingawa kuna wachezaji watatu kutoka ligi ya Premier League ya Uingereza lakini Kapteni Harry Kane hayupo kwenye orodha hiyo licha ya kushinda kiatu cha mfungaji bora kwenye kombe la dunia mwaka jana.
Mchezaji wa Liverpool Virgil van Dijk ,Chelsea N'Golo Kante na Eden Hazard ndiyo waliyochaguliwa kuingia kwenye orodha hiyo.
Cristiano Ronaldo ni moja kati ya wachezji walio orodhishwa akiwa na record ya kuibgia mara 13.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ureno ambaye kwasasa anakipiga Juventus, ameisaidia clu yake za zamani ya Real Madrid kushinda kikombe cha UEFA champions League mara tatu mfululizo.
Nyota wa Barcelona Lionel Messi ameorodheshwa mara 10 mfululizo kwenye kikosi hicho wakati mchezaji wa Paris St-Germain Kylian Mbappe ni moja kati ya wachezji wapya waliongia kwenye orodha hiyo ambao ni Marc-Andre ter Stegen, Van Dijk, Raphael Varane, na Kante.
Uefa.com XI:
- Marc-Andre ter Stegen (FC Barcelona & Germany)
- Sergio Ramos (Real Madrid CF & Spain)
- Virgil van Dijk (Liverpool FC & Netherlands)
- Raphael Varane (Real Madrid CF & France)
- Marcelo (Real Madrid CF & Brazil)
- N'Golo Kante (Chelsea FC & France)
- Luka Modric (Real Madrid CF & Croatia)
- Eden Hazard (Chelsea FC & Belgium)
- Kylian Mbappe (Paris Saint-Germain & France)
- Cristiano Ronaldo (Real Madrid CF/Juventus & Portugal)
- Lionel Messi (FC Barcelona & Argentina)