- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORTS: TFF YAWAFUNGIA WACHEZAJI WATANO WA YANGA NA MBEYA CITY
Kamati ya Utendaji ya ya saa 72 ya Bodi ya Ligi Tanzania imewafungia Wachezaji wa Mbeya City (Kelvin John na Majaliwa Shaban) na Yanga Sc (Mrisho Ngasa ,Ramadhani Kabwili na Cleafas Sospeter miezi mitatu(3) na Faini ya kiasi cha Shilingi 500,000 kila mmoja kwa kosa la kugoma kuingia vyumbani.
Hatua hii imekuja leo Januari 22, 2020 mara baada ya Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Januari 20, 2020 kupitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi na kufanya uamuzi huo
Klabu ya Tanzania Prisons na Yanga Sc zimepigwa Faini ya Tsh.500,000/=(Laki Tano) kila mmoja kwa kosa la kutokuwakilisha vikosi vya timu zao kwenye kikao cha maandalizi ya mchezo katika mechi hiyo iliyochezwa Disemba 29,2019 katika Uwanja wa Samora mjini Iringa.
Klabu ya Yanga Sc imetozwa faini ya sh. 500,000 kutokana na Washabiki wa timu yake kurusha chupa za maji kuelekea uwanjani na pia wakati wa mapumziko washabiki hao waliwarushia chupa za maji waamuzi wakati wanaelekea vyumbani katika mechi hiyo Januari 04,2020