- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORTS: RUFAA YA MANCHESTER CITY YAPOKELEWA NA MAHAKAMA YA USULUHISHI
Club ya Manchester City imekata rufaa kupinga adhabu ya kufungiwa kutoshiiriki Mashindano ya Barani Ulaya ( UEFA) katika mahakama ya usuluhishi wa migogoro ya michezo(Court of Arbitration for Sport (CAS))
Mahakama hiyo imekiri kupokea rufaa ya Manchester City na kuahidi kuifanyia kazi kikamilifu baada ya jopo la mahakama hiyo litakapokutana.
Taarifa ya Mahakama hiyo Imesema kuwa City Wamefungua Kesi dhidi ya Shirikisho la Soka Barani Ulaya (UEFA).
City imepigwa marufuku kushiriki katika ligi ya mabigwa Ulaya kwa misimu miwili ijayo(2020-2021) baada ya kupatikana wamekiuka sheria za Uefa zinazoambatana na masuala ya fedha na leseni.
Mabingwa hao wa ligi ya Premier pia wamepigwa faini ya £25m.
Bodi ya udhibiti wa masuala ya fedha ilisema kuwa City imevunja sheria kwa kuweka kiwango cha juu zaidi cha fedha katika mapato yake ya ufadhili kwenye hesabu zake na katika ripoti ya fedha iliyowasilishwa kwa Uefa kati ya 2012 na 2016 ikionesha kwamba hawakupata hasara wala faida", na kuongeza kwamba klabu hiyo haikushirikiana na wachunguzi".
Imesemekana kwamba City huenda pia ikapunguziwa pointi katika ligi ya Premier kwasababu sheria ya udhibiti wa masuala ya fedha katika ligi ya Premier kwa kiasi kikubwa inafanana na Uefa japo hazifanani moja kwa moja.
"baada ya jopo kuundwa, tutatoa utaratibu ukiwemo kuziita pande mbili husika na kuanzwa kwa kesi kusikilizwa" baada ya hapo Jopo litatoa ushindi kwa upande husika mara baada ya kuwasikiliza wote" imesema sehemu ya taarifa ya CAS