- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORTS: REAL MADRID YATANDIKWA KICHAPO CHA MABAO 7 - 3 DHIDI ATLETICO MADRID
Miamba ya soka nchini hispania Real Madrid jana imechezea kichapo cha mabao 7 - 3 dhidi ya mahasimu wao Atletico Madrid katika mchezo wa kujiandaa na msimu ujao wa 2019/2020 mchezo uliopigwa mji wa New Jersey nchini Marekani.
Mshambuliaji wa Atletico Madrid Diego Costa alifanikiwa kufunga mabao 4 katika mchezo huo kabla ya baaadae kutolewa njee.
Costa alianza kuifungia timu yake kunako dakika ya kwanza ya mchezo na akakamilisha kufunga hat-trick dakika ya 45 kwa mkwaju wa penati.
baadae Costa akaifungia club yake bao la 6 na kutimiza maboa 4 kabla ya mchezaji wa Real Madrid Dani Carvajal kuzawadiwa kadi nyekundu kwa kuanzisha ugomvi dakika ya 61.
Madrid walifungwa mabao 6 - 0 kabla ya kuliona lango la Atletico Madrid kupitia Nacho na baadae Karim Benzema na Javier Hernandez wakafunga goli moja moja.
Gareth Bale ambaye anatarajia kuondoka katika club hiyo na kujiunga na club ya china ya Jiangsu Suning, alitokea benchi kwenye dakika ya mwisho ya 30.
Madrid ambayo imetumia zaidi ya Paundi £300m msimu huu kwenye usajili wa kina Eden Hazard na Luka Jovic imeshindwa kutoka na matokeo chanya kwenye mechi za kujianda na msimu ujao .