- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORTS: POLISI WATOA WARANTI YA KUCHUNGUZWA DNA YA RONALDO
Mshambuliaji wa club ya Juvetus ya Nchini Italia Cristiano Ronaldo ameendelea kukubwa na misukosuko ya kashifa za Kingono baada ya Polisi mjini Las Vegas kutoa waranti ya kuchunguzwa kwa chembe chembe za vinasaba (DNA) kama sehemu ya uchunguzi wa madai ya ubakaji dhidi ya mwanamke mmoja Raia wa Marekani Kathryn Mayorga
Kwa mujibu wa Jarida la Wall Street limeripoti kuwa waranti hiyo imewasilishwa siku za hivi karibuni katika mahakama za Italia.
Ronaldo amekuwa akanusha kwamba alimshambulia mwanadada Kathryn Mayorga katika mgahawa mmoja mjini Las Vegas hotel mwaka 2009.
Wakili wa Mchezaji huyo Bw. Peter S. Christiansen amesema ''Bwana Ronaldo amekua akishikilia usemi kuwa yale yaliyotokea Las Vegas mwaka 2009 ni mambo ya watu wawili waliyokubaliana, kwa hiyo bila shaka chembe chembe za DNA zitapatikana, kwa hiyo sioni haja ya polisi kutoa ombi hilo kama sehemu ya uchunguzi wao,''
Gazeti la Der Spiegel la Ujerumani ambalo lilikuwa la kwanza kuangazia taarifa hiyo mwezi Oktoba, lilisema kuwa Bi Mayorga aliandikisha ripoti katika kituo cha polisi cha Las Vegas muda mfupi baada ya kufanyika kwa tukio linalodaiwa.
Der Spiegel lilisema kuwa mwaka 2010, Mayogra aliafikiana na Ronaldo kutatua suala hilo nje ya mahakama ambapo alilipwa dola 375,000 ilisizungumza hadharani madai hayo.
Mawakili wake sasa wanahoji kuwa makubaliano hayo hayakuwa rasmi.
Wakili Christiansen amewahi kusema kuwa mteja wake hakukataakutia saini makubaliano hayo "sababu zilizomfanya kufikia uamuzi huo zimepotoshwa".
Aliongeza: ''Hatua hiyo haimaanisha amekiri kuwa na makosa."
Bi Mayorga alipata ujasiri wa kuzungumzia masaibu yake kutokana na kampeini ya #MeToo movement, ambayo imekuwa ikiendeshwa mtandaoni.
Ronaldo alihamia Juventus kutoka Real Madrid mwezi Julai kwa kima cha euro 99.2.
Ameshinda tuzo ya Ballon d'Or - ambayo hupewa mchezaji bora wa soka duniani - mwaka 2008, 2013, 2014, 2016 and 2017.
Nyota huyo wa kimataifa wa Ureno aliwahi kupinga madai dhidi yake kama "taarifa ghushi" na baadae mwezi Oktoba akatoa taarifa kupitia mtandao wake wa Twitter ambapo alipinga "vikali" suala hilo.
Wakili wake anadai kuwa stakabadhi za uchunguzi zilizotumiwa na gazeti la Der Spiegel ''ni za kubuniwa" lakini gazeti hilo linasema "halina sababu" ya kutilia shaka uhalisia wake.