Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 9:36 am

SPORTS NEWS : LIGI YETU HAITAKI UFUNDI HATA KIDOGO-JULIO

Huyoo ndiye Julio bwana anakwambia ukileta ufundi umekaa "yani kama Chandimu"

Kocha wa Dodoma FC, Jamhuri Kihwelo 'Julio' amesema ligi ya daraja la Kwanza haina staili ya uchezaji kinachotakiwa ni kufunga ili timu ipate alama tatu tofauti na Ligi Kuu yenye mifumo na burudani kwa mashabiki

Julio amefunguka na kudai ligi ya FDL ni ngumu kwa kocha kuweka mfumo unaeleweka kutokana na kila kundi timu inatakiwa kupanda moja, hivyo kinachofanyika ni kuweka imara safu ya ushambuliaji

"Staili, mifumo na burudani huku havitakiwi kinachotakiwa ni kufunga uongoze kundi badae kupanda la sivyo ukicheza tu inakula kwako, burudani ya soka utaipata ligi kuu ambako timu ni nyingi na mechi ni nyingi,"alisema Julio

"Ninachoshukuru Mungu ni kwamba nimefanikiwa kufundisha timu za ligi kuu kama Mwadui FC niliyoipandisha mwenyewe na Simba, najua ugumu upo FDL ambako huwezi kuwa na mfumo unaoeleweka,"aliongeza

Licha ya kukiri kwamba FDL kuna wachezaji wenye haja ya kuonja utamu wa Ligi Kuu, lakini bado kuna changamoto ya kucheza soka la kisasa kwa maana ya mfumo wa kocha kuonekana

Timu ya Julio kwasasa inashika nafasi ya pili kwenye kundi C baada ya kucheza michezo minne na kuvuna alama tisa huku ikifungwa mchezo mmoja dhidi ya Alliance School kwa bao moja kwa bila