Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 9:43 am

SPORTS NEWS : KIERAN GIBBS ATUA WEST BROM

Timu ya West Brom imekamilisha usajili wa beki wa kushoto kutoka Arsenal Keiran Gibbs,kwa mkataba wa miaka minne,kwa ada ya uhamisho inayoaminika kuwa ni £7m.

Bibbs ambaye alianza kuitumikia Arsenal akiwa na umri wa miaka 14,anakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa na West Brom katika dirisha la usajili msimu huu

"wamefanya usajili mzuri na nafikiri kuwa huu ni usajili sahihi kwangu"alisema Gibbs

Keiran Gibbs akiwa katika Uzi wa timu yake mpya ya West Brom mapema leo hii

Beki huyo ameitumikia timu yake ya taifa ya Uingereza mara kumi tu,huku mechi yake ya mwisho ikiwa dhidi ya Ufaransa ambapo uingereza ilishinda 2:0 katika mechi hiyo ya kirafiki iliyochezwa November 2015

"Tumeongeza mchezaji mwingine mwenye ubora,anacheza timu ya taifa mwenye uzoefu katika ligi kuu na ngazi ya ligi ya mabingwa pia"alisema mwenyekiti wa West Brom,John Williams.


Tabasamu la Gibbs akiwa na timu yake ya zamani ya Arsenal

Tangu mwisho wa msimu uliopita West Brom imemsajili Jay Rodriguez 28,kwa ada ya uhamisho £12m,ikamsajili tena mlinzi wa Misri Ahmed Hegazi 27 kwa mkopo wa muda mrefu,bado ikaendelea kuimarisha kikosi ikamsajili tena Gareth Barry, 36,kwa ada ambayo haikutajwa

Mchezaji kutoka Scotland Oliver Burke alijiunga West Brom wiki iliyopita akitokea ujerumani katika timu ya RB Leipzig kwa mkataba wa miaka mitano,kwa ada ya uhamisho ya £15m.

West Brom pia imemsajili mshambuliaji kutoka China Yuning Zhang,20 ambaye ameanza kwa mkopo katika timu ya Werder Bremen nchini Ujerumani