- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORTS NEWS : HASSANI BANYAI -TUTASHINDA MECHI ZIJAZO
Baada ya kupoteza michezo miwili mfululizo ya ligi kuu ya Tanzania bara, kocha wa Njombe Mji Hassan Banyai amesema bado matumaini ya kufanya vizuri yapo kwani mpaka sasa ligi bado ni mbichi
Timu ya njombe Mji ambayo imepanda daraja mwaka huu,imejikuta ikianza vibaya baada ya kupoteza michezo miwili mfululizo,lakini kocha wa timu hiyo anasema bado mapema sana,kwani timu yake ana imani itafanya vyema
"Timu ina vijana wengi bado wanahitaji kutengenezwa vizuri,mechi zipo nyingi tutafanya vizuri,ligi bado nafikiri tunaendelea kujipanga"anasema Banyai
Njombe Mji ilipoteza mchezo wake wa ufunguzi wa ligi dhidi ya Tanzania Prison kwa kufungwa 2-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa sabasaba mkoani njombe,ikapoteza mchezo mwingine dhidi ya Yanga kwa bao 1-0 katika dimba lao la sabasaba siku ya jumapili
Kocha Banyai ameiambia muakilishi.com kuwa bado ana imani kuwa Njombe mji itafanya vizuri,kwani hata bingwa wa ligi kuu mpaka sasa hawezi kujulikana kutokana na ugumu wa ligi na tofauti ya alama baina ya timu na timu
"Timu zipo nyingi na mizunguko ni miwili,kwahiyo bado tunafanya maandalizi ya kutosha kuelekea michezo mingine kwa hiyo mapema,hata bingwa wa ligi huwezi kumtabiri kwa muda huu"aliongeza kocha huyo wa Njombe Mji
Njombe mji itasafiri kwenda mkoani Mbeya kukipiga dhidi ya Mbeya city katika dimba la sokoine katika mchezo wa mzunguko wa tatu wa ligi kuu bara.