Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 12:25 pm

SPORTS NEWS : FULLTIME ,STARS 2-0 BOTSWANA

Timu ya taifa ya Tanzania imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Botswana mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliyopo katika ratiba ya FIFA uliyopigwa katika uwanja wa Uhuru na kuhudhuriwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harisson Mwakyembe na Rais wa TFF, Wallace Karia.

Mabao ya Stars yakifungwa na kiungo wa kimataifa wa Tanzania anayekipiga nchini Morocco katika Klabu ya Difaa El Jadidi inayoshiriki Ligi Kuu ya nchi hiyo Simon Msuva.

Saimon Happygod Msuva ameipatia Stars mabao katika dakika ya 20 ya kipindi cha kwanza na kipindi cha pili katika dakika ya 60 huku akionekana kufanya vizuri zaidi katika mchezo huo.

.

Hizi ndizo takwimu za kipindi cha kwanza, Botswana wameongoza kwa umiliki wa mpira




TAKWIMU: Hizi ndizo takwimu za mchezo baada ya kipindi cha pili: Tanzania 2-0 Botswana (Msuva 5?, 61)



Katika kikosi hicho cha kocha Salum Shabani Mayanga, kimefanya mabadiliko kadhaa wakati wa mchezo huo kwa kumtoa Mzamiru Yasin na kuingia, Raphael Daudi katika kipindi cha pili na kutoka Shiza Ramadhani Kichuya na nafasi yake kuchukuliwa na Faridi Musa, Himid Mau akitoka na kuingia Said Hamisi Ndemla pia mfungaji wa mchezo huo Simon Msuva ikitoka na Mbwana Samatta akitoka pia.