- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORTS NEWS : BUSWITA ALITAKIWA KUWAJIBISHWA-ULIMBOKA
Mchezaji wa zamani wa klabu ya Simba sc Ulimboka mwakingwe amelifungukia Sakata la mchezaji Pius Buswita kwa kusema mazoea yanazaaa tabia hivyo mchezaji buswita alitakiwa kuadhibiwa kutokana na sheria zinavyosema
Ulimboka amesema mchezaji kusaini timu mbili sio suala la kawaida hivyo sheria zilitakiwa kufuatwa kama inavyotakiwa na sio kulimaliza sakata lake kwa kumruhusu kujiunga na moja ya timu alizosaini ambayo ni Yanga
“tabia huzaa mazoea,Buswita alitakiwa asicheze timu yoyote na sheria zingefuatwa ,sheria zipo nashangaa sheria zipo lakini azifuatwi”alisema Ulimboka
Ulimboka ameitupia lawama Tff kwa kushindwa kusimamia sakata la buswita na hatimaye mchezaji huyo kuruhusiwa kujiunga na yanga badala ya sheria kufuatwa kama inavyotakiwa kulingana na kosa alilofanya
“ni aibu mchezaji amesaini timu mbili wanamwambia ajiunge na yanga kasha arudishe pesa ya usajili wa timu nyingine hakuna kitu kama hiki uliona wapi”alifunguka Ulimboka
Buswita alitokea mbao fc na kusaini kunako Simba na Ikumbukwe mwishoni mwa mwezi Juni,Simba walitangaza kumsainisha Buswita kabla ya kuibukia Yanga ambayo walimpa mkataba wa miaka miwili.
Kwa sasa Mchezaji huyo ameruhusiwa kujiunga na yanga,lakini kabla ya kucheza mchezo wowote anatakiwa kurejesha fedha kiasi cha million 10 kwa timu ya simba ndipo aanze rasmi kuitumikia timu yake ya yanga.