- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORTS NEWS : BUNDUKI 21 ZITAKAZOIANGAMIZA MALAWI
Kocha wa timu ya taifa ya soka ya wanaume Taifa Stars, Salum Mayanga jana ametaja kikosi cha wachezaji 21 kitakachoivaa Malawi Oktoba 7 mwaka huu kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar esalaam ikiwa ni mchezo wa kirafiki wa Kalenda ya FIFA.
Kikosi kamili cha Taifa Stars.
Kikosi hicho kinachotarajiwa kuingia kambini Ijumaa Oktoba mosi, mwaka huu kina makipa Aishi Manula (Simba SC), Ramadhani Kabwili (Young Africans) na Peter Manyika (Singida United).
Walinzi ni Gadiel Michael (Young Africans), Boniphas Maganga (Mbao FC), Abdi Banda (Baroka FC/Afrika Kusini), Kelvin Yondani (Young Africans), Salim Mbonde (Simba SC), Erasto Nyoni (Simba SC) na Adeyum Ahmed (Kagera Sugar).
Viungo wa kati ni Himid Mao β Nahodha Msaidizi (Azam FC), Hamis Abdallah (Sony Sugar/Kenya), Mzamiru Yassin (Simba SC) na Raphael Daud (Young Africans).
Viungo wa pembeni ni Saimon Msuva (Difaa El Jadidah/Morocco), Shizza Kichuya (Simba SC), Abdul Hilal (Tusker/Kenya), Ibrahim Ajib (Young Africans) na Morel Orgenes (FC Famalicao/Ureno).
Washambuliaji ni Mbwana Samatta (KRC Genk/Ubelgiji) na Mbaraka Yussuph (Azam FC).