Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 9:52 am

SPORTS: MOURNHO "NIMEKATAA OFA TATU TANGU NIONDOKE MAN U"

Aliyekuwa mkufunzi wa zamani wa club ya Manchester United Bw. Jose Mourinho anadai kuwa amekataa ofa tatu za kuwa kocha mkuu tangu alipotimuliwa kazi na Man United huku akipinga madai kwamba anapendelea sana mfumo wa kupaki mabasi.

''Filosofia yangu inategemea. Ningependa kuwa katika klabu ambayo itanipatia mazingira sawa na yale ambayo mkufunzi wa liverpool anapata na mwenzake wa Manchester City''.

''Tayari nimekataa ofa tatu za kazi kwasababu nahisi sio ninachotaka''.

Maourinho ambaye aliiongoza Man United kushinda kombe la ligi pamoja na lile la bara Ulaya , anaeleweka kuwa na kandarasi ya kuondoka katika klabu hiyo ambayo inamzuia kuzungumzia kuhusu kuondoka kwake katika klabu hiyo.

Lakini alizungumzia kuhusu maswala kadhaa akiwa mgeni katika chombo cha habari za michezo cha Bein Sports:

Raia huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 55 alibwaga manyanga baada ya klabu hiyo kusema kuwa hakuna hatua aliyopiga kutokana na matokeo duni ya mechi , mtindo ama hata kuwaimarisha wachezaji chipukizi.

Tokeo la picha la jose mourihno

Laikini Mourinho alisisitiza kuhusu mchezaji mmoja ambaye alimtaka kutomkosoa huku Mourinho akihisi kwamba ni ishara ya wachezaji wa kisasa kuwa na hisia nyingi.

''Hivi majuzi nilipokuwa nikifunza mchezaji mmoja aliniambia tafadhali unaponikosoa nikosoe katika faragha sio mbele ya wachezaji wengine'' , alisema.

''Nilimuuliza kwa nini? alinijibu ''kwa sababu kwa hadhi yangu mbele ya wachezaji wengine unaponikosoa sihisi vyema''.

''Siku hizi lazima uwe mwerevu katika kuwasoma wachezaji wako, na kujaribu kuunda mazingira bora''.

Alilinganisha hali hiyo na ile ya mshambuliaji wa Chelsea Didier Drogba , ambaye alishirikiana naye katika uwanja wa Stamford Bridge aliposhinda ligi mara mbili 2005 na 2006.

''Drogba ni mchezaji ambaye unapozidisha shinikizo kwake ndipo anavyozidi kuimarika katika mchezo wake'', alisema Mourinho.

''Kuna wachezaji ambao unapowapatia shinikizo ndiposa wanapozidi kuimarika''.

''Kuna wengine ambao mafikra yao na tabia zao sio nzuri. Walilelewa katika mazingira tofauti , kwa wao kufikia kilele cha soka kila kitu walipata kwa urahisi. Kuna wengine hawatoa hisia sawa, hutoa maneno machafu na mara nyengine wengine ni hatari''.