- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORTS: MO DEWJI AMKINGIA KIFUA WAZIRI MWAKYEMBE SAKATA LA HISA KWEYE VILABU
Mwenyekiti wa Baraza la wazamini wa Club ya Simba Sport Club Mohamed Dewji ameonesha kusikitishwa juu ya taarifa za Uwongo zinazosambaa mitandaoni na kwenye vyombo vya habari zikisema kuwa Waziri wa Habari, Sanaa utamaduni na michezo Harrison Mwakyembe kuwa ameanzisha utaratibu mpya wa mwekezaji kuwa na 49% na wanachama 51% ya hisa katika umiliki wa vilabu hapa nchini, taarifa ambayo Mo ameikanusha.
"Nimesikitishwa na mijadala mitandaoni ya kumshutumu Waziri Mwakyembe kwamba ameanzisha utaratibu mpya wa mwekezaji kuwa na 49% na wanachama 51% ya hisa. Ndugu zangu, si kweli. Utaratibu huu upo tangu 2017 kisheria na sisi simba tulikubali" amesema MO kupitia ukurasa wake wa Twitter
Tajiri huyo kijana namba moja Afrika amesema kuwa yeye kama mwekezaji na mwanachama wa simba hataondoka katika club hiyo na kwa sasa wamefikia pazuru mazungumzo ya wao na serekali.
"Waziri Mwakyembe alituruhusu SIMBA tuendelee na mwekezaji mmoja. Ndugu WanaSimba Mimi nipo na niko na nyinyi, siendi popote. Na sasa tumeishazungumza na Serekali na mazungumzo ni mazuri. Nawasihi WanaSimba wote twendeni tukaishangilie Timu ya Taifa na tukutane Simba Day tarehe 6. Tulianza vizuri na Serikali na tutamaliza vizuri na Serikali"