- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORTS: MNYAMA SIMBA AUWA MTU MABAO 3 - 0 UWANJA WA TAIFA
Club ya wekundu wa Msimbazi Simba Sport Club leo imewakosha mashabiki wake wengi baada ya kuibuka na ushindi wa Mabao 3 - 0 dhidi ya JS Saoura kwenye mchezo wa kwanza wa makundi Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Emmanuel Okwi na Meddie Kagere (2) yameifanya timu hiyo kuongoza Kundi D.
dakika 45 za kipindi cha kwanza za Simba SC ilikwenda mapumziko ikiwa inaongoza bao 1-0 lililofungwa mwishoni na Emmanuel Okwi.
Mganda Juuko Murshid alionekana kufiti kwenye nafasi ya Erasto Nyoni ambaye ni majeruhi kwa kucheza kwa maelewano mazuri na Paschal Wawa ambaye ni kama kiungozi kwenye safu ya ulinzi ya Simba.
Mabeki hao walikuwa wakifanya kazi ya ziada kwa kuwasaidia walinzi wa pembeni wa Simba pindi ambapo walikuwa wakishindwa kuwadhibiti washambuliaji wa JS Saoura. Safu ya ulinzi ya Simba SC ilikuwa ikiundwa pia na kina Nicholus Gyan na Mohammed Hussein 'Tshabalala'. Mabeki wa kati, Pascal Wawa na Juuko Murshid walionekana kuwa na maelewano mazuri kwenye kikosi cha Simba.