- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORTS: MAN CITY YAAHIDI KUKATA RUFAA ADHABU YA KUTOSHIRIKI UEFA
Klabu ya Manchester City ya nchini Uingereza imepigwa marufuku kushiriki kwenye ligi ya mabigwa barani Ulaya(UEFA Champions League) kwa misimu miwili ijayo na kutozwa faini ya £25m baada ya kukiuka sheria za Uefa kwenye masuala ya fedha na leseni(Financial Fair play).
Manchester City imesema kwamba hatua hiyo ni jambo la kukatisha tamaa lakini halikuwashangaza na wameahidi kuikatia rufaa adhabu hiyo katika katika mahakama ya usuluhishi wa migogoro ya michezo.
Bod ya udhibiti wa masuala ya fedha imesema City imevunja sheria kwa kuweka kiwango cha juu zaidi cha fedha katika mapato yake ya ufadhili kwenye hesabu zake na katika ripoti ya fedha iliyowasilishwa kwa Uefa kati ya 2012 na 2016 ikionesha kwamba hawakupata hasara wala faida", na kuongeza kwamba klabu hiyo haikushirikiana na wachunguzi".
Imesemekana kwamba City huenda pia ikapigwa nyundo nyingine kwa kupunguziwa alama katika ligi ya Premier kwasababu sheria ya udhibiti wa masuala ya fedha katika ligi ya Premier kwa kiasi kikubwa inafanana na Uefa japo hazifanani moja kwa moja.
Hata hivyo, adhabu hiyo haitakuwa na athari zozote kwa timu ya wanawake ya City.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Manchester City: "Klabu hiyo imekuwa ikifikiria umuhimu wa kuwa na bodi huru na kufuatwa kwa mchakato usiopendelea upande wowote kuangalia ushahidi wao ulio wazi.
"Disemba 2018, mchunguzi mkuu wa Uefa alisema wazi vikwazo ambavyo anataka City iwekewe hata kabla ya uchunguzi kuanza kufanywa.
"Kasoro na udhaifu uliopo katika mchakato wa Uefa kwenye uchunguzi alioongoza, hakukuwa na shaka na matokeo ya uchunguzi huu. Klabu hii awali ilikuwa imewasilisha malalamiko yake kwa bodi ya nidhamu ya Uefa, ambayo yaliidhinishwa na mahakama ya usuluhishi wa migogoro ya michezo.
"kwa maneno rahisi, hii ni kesi iliyowasilishwa na Uefa, ikashtakiwa na Uefa na aliyetoa uamuzi ni Uefa. Kwa mchakato wa kibaguzi aina hii ambao umemalizika, klabu hii sasa itatafuta hukumu isiyopendelea upande wowote haraka iwezekanavyo na hivyo basi, kwanza kabisa itaendelea na mchakato wake katika mahakama ya usuluhishi wa migogoro ya michezo bila kuchelewa."
City imepangwa kucheza na Real Madrid katika timu 16 za mchujo za ligi ya mabingwa huku mchuano wa kwanza ukiwa ni Februari 16 katika uwanja wa Bernabeu.
Rais wa La Liga Javier Tebas iliisifu Uefa kwa kuchukua hatua stahiki.
"Kuhakikisha utekelezaji wa sheria ya udhibiti wa fedha na kutoa adhabu kwa wanaokiuka sheria hiyo ni jambo la msingi kwa hatma ya mpira wa kandanda," amesema.
"kwa miaka mingi tumekuwa tukitoa wito wa kuchukuliwa kwa hatua muafaka dhidi ya Manchester City na Paris Saint-Germain, na hatimaye tumepata mfano bora na ni matumaini yetu kwamba hili litaendelezwa. Ni kheri kuchelewa kuliko kutochukuliwa kwa hatua kabisa."