- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORTS: MADRID NA HOTSPURS ZAANZA VIZURI KAMPENI YA UEFA
Club ya Tottenham Hotspurs imefanikiwa kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Borussia Dortmund kutoka nchini Ujerumani katika uwanja wa taifa wa Uingereza Wembley
Kunako Dakika 47' Mkorea Heung-Min Son ndie aliyeanza kuwapatika Spurs, goli la kuongoza , beki Jan Vertonghen akaongeza goli la pili katika dakika ya 83.
Naye Mshambuliaji raia wa Hispania Fernando Llorente, alihitimisha kazi kwa goli la tatu katika dakika ya 86.
Kwa Upande wao mabingwa watetezi wa michuano hiyo Real Madrid, wakiwa ugenini nchini Uholanzi katika dimba Johan Cruijff Arena, wamepata ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya wenyeji wao Ajax.
Mshambuliaji wa Real Madrid, Karim Benzema, aliipatia timu yake goli la kuongoza katika dakika ya 60, Ajax walichomoa goli hilo kupitia kwa Hakim Ziyech katika dakika ya 75,
Zikisalia dakika tatu mchezo kumalizika Marco Asensio, alifunga goli la pili na la ushindi kwa Real Madrid.
Michezo mingine ya michuano hiyo itaendelea wiki ijayo tarehe 19, Liverpool watakuwa wenyeji wa Bayern Munich, huku Lyon wakiwalika Fc Barcelona.
Tarehe 20, Atletico Madrid watacheza na Juventus, nao Schalke 04 wakiwapokea Manchester City.