- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORTS: KIPA WA YANGA BENO KAKOLANYA AWASHTAKI YANGA TFF
Mwanasheria wa kipa wa Yanga, Beno Kakolanya, Bw. Leonard Richard, amesema wameamua kupeleka barua ya kuvunja mkataba katika Shirikisho la Soka nchini Tanzania(TFF), ili mchezaji huyo aangalie maisha mengine nje ya klabu hiyo, huku akidai kuwa Yanga inaonesha haina lengo zuri na kipa huyo.
Kakolaya amekuwa kwenye Mgogoro wa Muda sasa na kocha wa timu hiyo, Mwinyi Zahera, huku akimuweka benchi kwa madai ya utovu wa nidhamu baada ya kuweka mgomo wa kujiunga na wenzake akishinikiza kulipwa stahiki zake.
Richard amesema aliamua kufanya mawasiliano na Kaimu Katibu wa Yanga, Omary Kaaya, pamoja na Kaimu Mwenyekiti, Samuel Lukumay, kwa ajili ya kufahamu nini kinaendelea na hatima ya mteja wake, lakini viongozi hao hawakupokea simu ya mwanasheria huyo juu ya kuhitaji majibu ya barua yao.
“Awali walituandikia barua kwamba Kakolanya hawadai Yanga, lakini mteja wangu anachohitaji ni kufahamu hatima ya maisha yake ndani ya kikosi cha timu hiyo, majibu walitakiwa kujibu wiki iliyopita lakini kila siku wamekuwa wakituzungusha.
“Kitendo cha kuwavumilia kwa miezi yote tangu Novemba hadi sasa, kwa jinsi wanavyotuzungusha kinaonyesha dhahiri kwamba Yanga hawamtakii mema mchezaji huyo, hivyo barua tayari imeshaandikwa kwahiyo kati ya leo mchana au jioni Ijumaa tutawasilisha TFF barua ya kuvunja mkataba,” alisema Mwanasheria huyo.
Alisema kabla ya kuchukua maamuzi hayo alijaribu kufanya mawasiliano na viongozi wa Yanga, baada ya kuzungumza na Kaaya na kumweleza kwamba kesi hiyo ipo mikononi mwa Lukumay ambapo naye hapokei simu.
“Nilijitahidi kufanya mawasiliano mara watueleze kwamba mwanasheria wao amesafiri na kutupiga kalenda, ilikuwa mwisho Jumanne iliyopita ila leo (jana) nimejaribu kupiga simu pia hakupokea, hivyo tumeamua kupeleka barua TFF kwamba Kakolanya sasa yupo huru,” alisema Richard.
Alieleza Yanga hawaoni umuhimu wa kipa huyo kutokana na kushindwa kutoa majibu ya barua yao, baada ya sakata lake hilo kuunguruma miezi minne sasa tangu Novemba, mwaka jana.