- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORTS: HII NDIO ORODHA YA VILABU 10 TAJIRI DUNIANI, MADRID YAONGOZA
Orodha ya vilabu tajiri zaidi duniani ambayo huchapishwa kila mwaka na kampuni ya kihasibu ya Deloitte Kuonesha thamani ya vilabu bila kujumuisha madeni.
Real Madrid imetajwa kuwa klabu tajiri zaidi duniani kwa kuwa na thamani ya pauni milioni 674.6
Club Barcelona nayo kutoka hispania imeipiku Club ya Uingereza ya Manchester United kwa kushika nafasi ya pili na kushuka hadi nafasi ya tatu.
Real Madrid ilishinda taji la ligi ya mabingwa kwa mara ya tatu mfululizo baada ya kuinyuka Liverpool mabao 3-1 mjini Kiev mwezi Mei mwaka uliopita.
Ushindi huo uliisadia Real kuongeza mapato yake na kuifanya kuwa timu yenye mapato makubwa mara kumi na mbili katika orodha ya Deloitte
Klabu hiyo ilishuhudia ukuaji wa biashara yake kwa pauni milioni 54.8, iliyojumuisha ongezeko la wadhamini,mapato ya uuzaji wa bidhaa zao na kuongezeka kwa ziara ya kabla mwanzo wa msimu.
Real Madrid imevuja rekodi kwa kukusanya mapato ya kibiashara ya jumla ya pauni milioni 356.2 kiwango ambacho kimeifanya kuwa klabu tajiri zaidi duniani ukilinganisha na vilavu vingine.
Dan Jones, mkuu wa kitengo cha uhasibu wa masuala ya michezo katika kampuni ya Deloitte, amesema: "matokeo bora ya Real Madrid mwaka 2017-18 yamechangia historia ya ufanisi wao uwanjani ikiwa ni pamoja na ushindi wa hivi karibuni wa mataji matatu ya ligi ya mabingwa.
Vilabu vya Bayern Munich na Manchester City vilisalia katika nafasi zao kwa miaka miwili iliyopita.
Paris St-Germain, Liverpool, Chelsea, Arsenal, na Tottenham Hotspur walishikilia nafasi ya sita hadi kumi.
Everton walishikilia nafasi ya 17, Newcastle United ya 19, na West Ham United nafasi ya 20.
Vilabu vyote 20 vilivyo kwenye nasi ya ''tano bora'' vinashiriki ligi kuu za mataifa ya bara ulaya, ikiwa ni pamoja na Italia iliyonyakua nafasi nne, nazo Ujerumani na Uhispania zikichangiavilabu tatu, huku Ufaransa ikisalia na nafasi moja.
Matokeo mengine yanajumuisha:
- Spurs wamepewa nafasi ya kucheza msimu kamili katika uwanja wa Wembley ambao umeona ongezeko la mapato ya siku ya siku kwa 54%
- Mapato ya Paris Saint-Germain yameshuka kwa miaka miwili mtawalia
- AS Roma na AC Milan wamerejea katika orodha ya 20 bora baada ya kuandikisha matokeo bora katika mashingano ya Uefa
- Mabingwa wa Uturuku Besiktas wamepata ufanisi mkubwa baada ya kuorodheshwa nambari 26.