- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORTS: HATIMAYE MZEE KILOMONI AVULIWA CHEO CLUB YA SIMBA
Dar es salaam: Uwongozi wa klabu ya Simba sport club ya Jijini Dar es salaam kupitia Afisa mkuu mtendani wao Crescentius Magori leo Julai 16, 2019 wametangaza rasmi kumuondoa kwenye sehemu ya baraza la wadhamini la klabu hiyo Mzee Hamisi Kilomoni.
Uwamuzi huu wa Simba umekuja Miezi kadhaa baada ya Mzee Kilomoni na Wenzake kuvutana kwa muda na uongozi wa klabu ya hiyo uliopo madarakani sasa kuhusu mabadiliko ya uendeshaji wa klabu hiyo nchini ya Mwenyekiti wa Baraza la Wazamini Mohamed Dewji.
"Hapa karibu tumekuwa na taarifa mbalimbali kuhusu Hamis Kilomoni kuwa mdhamini wa klabu yetu ya Simba"-Crescentius Magori, Mtendaji Mkuu Simba SC.
"Hamisi Kilomoni ambaye alikuwa ni mdhamini wa Baraza la Simba, amekuwa akipita kwenye vyombo vya habari akieleza habari za klabu yetu."
"Kuanzia leo tunatangaza kuwa Mzee Kilomoni sio tena mdhamani wa Baraza la Simba na mkataba wake haupo tena, maana mkataba ulimalizika October 2017."
Bw. Magori ameongezea kuwa Simba imemaliza sakata la Mzee Kilomoni na kwamba hawatalizungumzia tena kitu chochote kinachomuhusu mzee huyo.
"Na kwa msisitizo zaidi maswala yake tumeyafunga leo hatutaliongelea tena swala lake, zaidi hatua za kisheria zitafata."