- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORTS: FAINALI KLABU BINGWA AFRIKA KURUDIWA TENA , YASEMA CAF
Shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika CAF, limeamuru mechi ya mzunguko wa pili ya fainali ya mashindano ya klabu bingwa Afrika, kati ya Esperance na Wydad Casablanca, kurudiwa kwenye uwanja huru, baada ya kumalizika kwa mashindano ya kombe la mataifa Afrika yanayofanyika mwezi huu nchini Misri.
Klabu ya Esperance ya Tunisia, ilikuwa imekabidhiwa kombe hilo awali, baada ya Wydad Casablaca kutoka Morocco, kuondoka uwanjani katikati mwa mechi kwa sababu ya kukosekana kwa tekonolojia ya VAR kuamua juu ya goli la kusawazisha lililokataliwa.
Mabingwa Esperance walikuwa wanaongoza kwa bao 1-0 katika mzunguko wa pili na 2-0 kwa ujumla wakati mechi hiyo iliposimamishwa, na baada ya ucheleweshaji wa dakika 90, mwamuzi alitoa ushindi kwa Esperance ambao ndiyo walikuwa wenyeji wa mechi hiyo ya marudio. Afisa wa Esperance amesema watapinga uamuzi huo kwenye mahakama ya kutatua mizozo ya kimichezo.