Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 11:59 am

SPORT: RAIS WA SHIRIKISHO LA SOKA CAF AKATAA KULIPWA MSHAHARA

Khartoum: Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) Ahmed Ahmed amekataa kulipwa mshahara wake kama rais wa shirikisho hilo ''Nimekataa kuchukua mshahara kwa sababu sio heshima kwa usimamizi mzuri'', aliambia BBC Sport. ''Mishahara wa wafanyikazi wote wa Caf kutoka wasimamizi hadi maafisa wakuu na rais ni lazima iwe na uwazi''.

Raia huyo wa Madagascar mwenye umri wa miaka 57 alisimamia mkutano wake mkuu katika shirikisho hilo siku ya Jumatatu kabla ya kufanyika kwa mkutano mkuu wa shirikisho la Fifa siku ya Alhamisi. Katika mkutano huo mambo muhimu yatakayo jadiliwa ni pamoja na kufanya mabadiliko katika Caf.

Tutachukua hatua ambayo itampendelea kila mtu ili kuhakikisha kwamba shindano hili linarudisha sifa yake na kuvutia raslimali mbali na ushaibiki mkubwa.

''Mabadiliko kuhusu usimamizi ni swala muhimu sana, kila mtu anapaswa kujua kinachotendeka'', alisema Ahmed.