- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORT NEWS: PENGO LA NIYONZIMA BADO KITENDAWILI KWA WANAJANGWANI
Dar es salaam: Pengo la mchezaji mashuhuri aliyekuwa anakipiga jangwani Haruna Niyonzima bado halijapata mrithi wake toka mchezaji huyo kuondoka klabuni hapo na kutimkia kunako klabu ya Simba Sport club, Kocha wa Yanga George Lwandamina,pamoja na viongoz wa Usajili wa klabu hiyo wako katika mtihani mzito kuliko wakati mwingine wowote wakitaka saini za nyota wawili Papy Kabamba Tshishimbi, wa Mbabane Swallows na Cletus Chama wa Zesco ya Zambia.
Lwandamina amesema kuwa katika wachezaji hao wawili anamuhitaji mchezaji mmoja ambaye ataziba vyema nafasi ya kiungo Haruna Niyonzima, aliyeondoka kwenye klabu hiyo na kujinga na mabingwa wa Kombe la FA, Simba
“Wote ni wachezaji wazuri nawajua vizuri lakini kuna tofauti moja ya uumri hapo ndipo nitakapopaangalia vizuri maana kuwa na mchezaji mwenye umri mdogo inakupa anakupa uhakika wa kuweza kupambana kwa asilimia 95 tofauti na mchezaji mwenye umri mdogo,”amesema Lwandamina.
Kocha huyo amesema anampa nafasi zaidi Chama, kwasababu ni mchezaji mzuri anauwezo wa kukaba lakini pia kuichezesha timu na kufanya mashambulizi hivyo ni mtu ambaye anampa kipaumbele.