Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 4:22 pm

SPORT NEWS: NGOMA "NIKO TAYARI KUISAINDIA YANGA BAADA YA KUPONA"

Dar es salaam: Mshambuliaji wa klabu ya Yanga Afrika Donald Ngoma anatarajia kujiunga na klabu yake kwenye mazoezi, Jumatatu, baada ya kupona tatizo lake la goti ambalo limemfanya akae nje kwa muda mrefu msimu uliopita wa mwaka 2016/2017

.

Ngoma aliongea na Muakilishi.com, kwa njia ya sim kuwa kwasasa amepona kabisa tatizo lake la goti na yupo tayari kuanza kuisaidia timu yake kwenye msimu ujao wa ligi ya Vodacom itakayoanza Agosti 26 mwaka huu.

“Nipo vizuri na fiti nimepona kabisa tatizo la goti, nilikuwa hapa hospitali Afrika Kusini kwa muda nikifanyiwa matibabu lengo ni kutimiza majukumu yangu vizuri nikiwa na Yanga,’amesema Ngoma.

Mshambuliaji huyo amesema anatarajiwa kurejea Dar es Salaam kesho Jumapili na Jumatatu atakuwepo kwenye kikosi cha Yanga ambacho kitaendelea na mazoezi kujiandaa na msimu ujao.

Amesema anataka kuifanyia mambo makubwa timu hiyo katika msimu ujao hivyo mabeki wa timu pinzani wajiandae kwani hatokuwa na msalie mtume.

Amesema anataka kulipa fadhila baada ya msimu uliopita kukaa nje kwa muda mrefu na kushindwa kuipigania timu hiyo ambayo alijiunga nayo misimu miwili iliyopita.

Ngoma hivi karibuni amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Yanga timu ambayo ameitumikia kwa mafanikio makubwa akitokea FC Platinum ya kwao Zimbabwe.