- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORT NEWS: MASHINDANO MAKUBWA YA MARATHON KUFANYIKA MONDULI.
MONDULI: Mashindano ya Riadha yenye Jina ‘Monduli Maasai Marathon’ yanatarajiwa kufanyika June 29, mwaka huu mjini Monduli mkoani Arusha.
Mratibu wa Mashindano hayo Cletus Pius Wilbert amesema mashindano hayo yataanzia eneo la uwanja wa Polisi ambapo kutakuwa na njia (route) tatu kulingana na umbali na kisha kuishia Uwanjani hapo.
Cletus amesema kutakuwa na mbio za kilomita 2.5 zilizopewa jina Nyangulo Fun Race, Km 5 Laigwanani VIP Race huku Km 21 zikiwa ni Morani. Washindi watazawadiwa zawadi mbalimbali akiwemo Ng’ombe mkubwa na mgeni rasmi ambaye atatangazwa baadaye.
Amesema maandalizi ya mashindano hayo yanaendelea vizuri ambapo kwa sasa kamati inaendelea kutafuta wadhamini mbalimbali ili kuweza kufanikisha zoezi hilo kwa ufanisi mkubwa.
Mratibu huyo amesema lengo kubwa la mashindano hayo ni kutangaza Wilaya ya Monduli ambayo ina fursa mbalimbali za utalii ambazo zinaweza kusaidia kuongeza mapato katika Halmashauri lakini pia kuhamasisha jamii kufanya mazoezi ili kuimarisha afya zao na kufufua riadha wilayani Monduli.
"Mashindano haya yanaandaliwa na LIVE HIGH COMPANY kwa kushirikiana na CAS MICROFINANCE LTD. Tumeaandaa zoezi hili ili kuitambulisha wilaya ya Monduli na fursa zilizopo",amesema.
Amesema Mbio hizo zitakazofanyika Monduli Mjini katika uwanja wa Polisi zitashirikisha washiriki mia tano [500] kutoka rika na jinsi mbalimbali wakiwemo vijana, watoto, wazee yakisindikizwa na kauli mbiu ‘MONDULI PAZURI, TAMBUA FURSA ZILIZOPO’.