- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORT NEWS: MANULA AIFANYA SIMBA KUIPIGIA MAGOTI AZAM FC
DAR ES SALAAM: UONGOZI wa Klabu ya Simba, umeipigia magoti Azam FC imruhusu Aishi Manula aweze kushiriki mazoezi na klabu hiyo mapema kwa kuwa bado ana mkataba wa mwezi mmoja na timu hiyo.
Inadaiwa kuwa Manula ameshamalizana na Simba kwa mkataba wa miaka miwili lakini hataweza kutangazwa rasmi kuwa mchezaji wa timu hiyo kwa kuwa bado mkataba wake na Azam FC haujamalizika.
Taarifa ambazo gazeti hili limezipata ni kuwa uongozi wa Simba umeiomba Azam FC kumruhusu Manula mapema ili akafanye mazoezi na kikosi hicho kilichopo Afrika Kusini ili kuepuka kesi kama ilivyokuwa kwa Hassan Kessy alivyokwenda Yanga.
Ulipotafutwa uongozi wa Azam FC kuzungumzia suala hilo ulisema kwa upande wao wanatambua kuwa Manula ni mchezaji wao hadi pale atakapomaliza mkataba na si vinginevyo.
“Manula bado ni mchezaji wetu hadi atakapomaliza mkataba wake, pia yeye mwenyewe ndiye anatakiwa aseme kama amemaliza mkataba ama la, lakini taarifa za Simba kufanya mazungumzo bado hazijanifikia,” alisema Mwenyekiti wa Azam FC, Idrisa Nassor.