- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORT NEWS: MAAMUZI YA AFCON YAFURAHISHA MASHINDANO YA UEFA CHAMPIONI
Morocco: Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON yameogezwa hadi timu 24 na kusogezwa katika tarehe za Juni na Julai lakini litaendelea kuandaliwa kila baada ya miaka miwili. Kwa sasa lilikuwa linazishirikisha timu 16.
Hayo ni kutokana na mapendekezo yaliyofanywa kuhusu mshindano hayo katika mkutano wa wadau ulioandaliwa mjini Rabat nchini Morocco. Uamuzi huo ni lazima upitishwe na kamati kuu ya Shirikisho la Kandanda Afrika β CAF, katika mkutano wake wa siku mbili mjini Rabat.
Mapendekezo hayo yanayosubiriwa kuidhinishwa rasmi, yalifanywa katika warsha kuhusu mustakabali wa wa kinyang'anyiro hicho ambayo kikao hicho kilijumuisha viongozi wakuu wa CAF.
Mshindano ya AFCON yamekuwa yakizusha utata kwa sababu ya kuandaliwa Januari, katikati ya msimu wa ligi kuu za kandanda Ulaya. Wachezaji wengi wa AFCON hutoka katika vilabu vya Ulaya na mara nyingi hujikuta katika hali ya vuta nikuvute kati ya klabu na nchi.
Ongezeko la timu linafuatia utanuzi wa dimba la ubingwa wa Ulaya β Euro mwaka jana, ambao wachambuzi wa Afrika walisema ulikuwa wa kufana.