- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORT NEWS: LIONEL MESSI KUAMUA KULIPA FAINI KUBWA AU KWENDA JELA MIAKA 2
Hispania: Mchezaji maarufu Duniani mwenye Rekodi kemkem kwenye anga za kandanda, na Mshindi wa ballon d'or mara tano Lionel Messi huenda akatozwa faini ya €255,000 ($285,000; £224,000), ambayo ni sawa na milioni 800,000 za kitanznia, Messi amepangiwa kulipa faini hiyo kama njia ya kukwepa kifungu cha kwenda jela kwa miezi 21.
Messi, pamoja na babake Jorge, walipatikana na hatia ya kuilaghai Uhispania jumla ya €4.1m kati ya mwaka 2007 na 2009.
Mahakama mjini Barcelona iligundua kwamba Messi na baba yake walitumia maeneo ya Belize na Uruguay ili kukwepa kulipa kodi.
Kando na huku hiyo ya kifungo jela, nyota huyo wa klabu ya Barcelona pia alitozwa faini ya €2m na babake €1.5m.
Lakini Messi na Baba yake Walijitolea kulipa €5m "kama malipo ya kufidia", kiasi ambacho ni sawa na kiasi cha kodi ambayo anadaiwa kukwepa kulipa pamoja na riba, Agosti mwaka 2013.
Rufaa ya Messi dhidi ya hukumu hiyo ilikataliwa na Mahakama ya Juu nchini Uhispania mwezi jana, ingawa muda wa babake kusalia gerezani ulipunguzwa kwa sababu alikuwa amelipa kiasi fulani cha kodi.