- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORT NEWS: CHELSEA YATWAA TAJI LA UEFA EUROPA LEAGUE
Club ya Chelsea ya Uingereza imenyakuwa taji la Europa League baada ya kuikung'uta Arsenal mabao 4 - 1 katika uwanja wa Baku nchini Azerbaijan.
Kiungo Machachari wa Club hiyo Eden Hazard amefunga mabao mawili ambayo huenda yakawa mabao yake na mechi yake ya mwisho kwa vigogo hao wa London Magharibi kwa msimu huu ambayo yamepelekea kuiadhibu Arsenal isifuzu kucheza katika Mashindano ya UEFA Champions League Mwakani 2019/2020.
Mshambuliaji wa Chelsea Olivier Giroud Ndio alikuwa wa kwanza kufungua kitabu cha Mabao kunako Dakika ya 49 kabla ya mshambuliaji wa Kibrazili Pedro dakika ya 11 baadaye kufunga goli la pili na kuifanya chelsea kuwa mbele kwa mabao 2 - 0.
Hazard baadaye akafunga bao lingine la tatu kwa Chelsea kupitia mkwaju wa Penaliti kwenye dakika ya 25 ya kipindi cha pili.
Chelsea walizawadiwa Penati baaada ya winga ya Arsenal Ainsley Maitland-Niles kumfanyia madhabi Girioud kwenye eneo la penati boxi.
Goli la pekee la Arsenal Limefungwa na Alex Iwobi kunako Dakika ya 69.
Hili ni kombe lake la kwanza kwa kocha Maurizio Sarri kushinda kikombe kikubwa katika maisha yake ya kisoka ya miaka 29 huku kukiwa na tetesi kuwa huenda akaondoka Stamford Bridge akajiunga na Juventus.