- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORT NEWS: BIGWA WA UEFA KUJULIKANA USIKU WA LEO
Uigereza: Michuano ya klabu bingwa barani ulaya inahitimishwa usiku wa leo mjini Cardiff, ambapo Timu ya Real Madrid itamenyana na Wababe wa Seria A Juventus, Timu zote hizi zikiwa nimabingwa katika ligi zao za ndani kwa kuchukua Taji za ligi, Real Madrid ndio mabingwa wa La liga kwa msimu huu 2016/2017 baada ya kulikosa kwa muda mrefu sambamba na Juvu kwa sasa ndio mabigwa wa Siria A wao wakiwa mabigwa wa ligi mara tatu mfululizo, Timu hizi zikiwa zimekutana mara 19 katika mashindano ya michuano ya barani ulaya zote zikiwa zimeshinda mechi 8 kwa kila mmoja, na Sare mara mbili, Juve amefunga mabao 21 na Real Madrid mabao 18. kwenye Ranking za UEFA Madrid inashika namba 1 na JUVE namba 9
Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane anakabiliwa na kibarua kigumu cha kuamua nani kati ya Gareth Bale na Isco atacheza katika fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya ya leo. Bale hajacheza tangu 23 Aprili lakini sasa yuko sawa kucheza.Isco, ambaye alijaza pengo lake naye amekuwa akicheza vyema sana na amefunga mabao matano katika mechi nane walizocheza hivi karibuni.
"Wote wawili ni wachezaji muhimu sana na kila mmoja anaweza kutoa maoni yake lakini hilo halitaniathiri," Zidane amesema.
Nae kocha wa club Juventus Max Allegri wachezaji wake wote pia wako sawa kucheza.
Gianluigi Buffon, Giorgio Chellini, Alex Sandro, Mario Mandzukic na Leonardo Bonucci walipumzishwa mechi ya mwisho ya Juve katika Serie A dhidi ya Bologna Jumamosi iliyopita.
Gianluigi Buffon, 39, atakuwa nahodha wa Juve katika mechi hiyo itakayochezewa Cardiff.
Buffon hajawahi kushinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya. "Itakuwa na maana kubwa sana kwangu," anasema mchezaji huyo, ambaye amechezea Italia mechi 168.
"Itakuwa siku ya furaha zaidi kwangu katika maisha yangu ya uchezaji, pamoja na Kombe la Dunia - kwa sababu itakuwa ni kama zawadi, baada ya safari ngumu yenye dhiki na visiki na bidii."