- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORT NEWS: BARCELONA YABEBA COPA DEL REY KWA KUICHAPA ALAVES 3 - 1
HISPANIA: Miyamba ya soka nchini Hispania jana ilibeba taji lake la 19 la Copa del Rey baada ya kuichakaza Alaves kwa kichapo cha mabao 3 - 1, wachezaji wa barcelona walikuwa kwènye kiwango cha juu kabisa kiasi kilichowafanya Alaves kukosa kupenya kwenye mlango wa Barcelona.
Barcelona ndio ilikuwa ya kwanza kuliona lango la Alves kupitia mshambuliaji wake hatari zaidi Duniani Lionel Messi, ambapo kunako Dakika ya 30' pasi murua kuto?a kwa mbrazili Neymar, Messi amefikisha mabao 54 kwenye msimu mzima wa 2016/2017, baada ya dakika chache Alaves walisawazisha baada ya Mchezaji wa Alves kuchezewa faulo na Iniesta, Dakika 45 Neymar aliiandikia Barcelona goli la pili na lakuongoza.
Barcelona waliendelea kuwapa presha wapinzani wao kwa kucheza kwenye final third ya Alaves ambapo sekundeg chache kabla ya mechi kwenda mapumzikoni kinda wa Barcelona Alcácer aliipatia Timu yake ya Barcelona goli la tatu na lakuongoza, baada ya mchezo kurudi mapunziko milango yote miwili ilikuwa migumu kufanya mabao kubaki kama yalivyokuwa, mpaka mpira unakwisha Barcelona ilikuwa inaongoza kwa kumiliki mpira kwa asilimia 73%.
Ushindi huu wa Barcelona umemsaidia kocha Luis Enrique kuondoka akiwa na taji, Barcelona ilitangaza kuachana na kocha wake mwishoni mwa msimu huu kwahiyo mchezo wa fainali wa Copa del rey ndio ulikuwa mchezo wake wa mwisho kuitumikia Barcelona baada ya miaka mitatu kuitumikia Barcelona.