- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORT: MOURINHO ATEULIWA KUWA KOCHA MPYA WA TOTTENHAM HOTSPUS
Aliyekuwa mkufunzi wa club za Manchester United, na Chelsea Jose Mourinho ameteuliwa na bodi ya club ya Tottenham Hotspus kuwa mkufunzi mpya wa club hiyo akichukua mikoba ya kocha wao wa muda mrefu Mauricio Pochettino ambaye alifutwa kazi siku ya jana jumanne.
Mourinho ambaye ni mkufunzi wa zamani wa club kubwa Duniani kama Chelsea, Real Madrid, Milan, Man united ametia saini kandarasi ya miaka 3 hadi mwisho wa msimu wa 2022-23.
''Jose ni mmojawapo wa wakufunzi mwenye utajiri mkubwa wa uzoefu sana katika soka'', alisema mwenyekiti wa Spurs Daniel Levy.
Jose Mourinho alidaiwa kuwa katika mazungumzo ya kuchukua mahala pake Mauricio Pochettino kama mkufunzi wa Tottenham.
Pochettino mwenye umri wa miaka 47 alifutwa kazi kama mkufunzi wa Spurs siku ya Jumanne baada ya kuhudumu katika klabu hiyo kwa kipindi cha miaka mitano akiisimamia klabu hiyo ya kaskazini mwa London.
Raia huyo wa Argentina aliiongoza Spurs katika fainali ya kombe la klabu bingwa Ulaya msimu uliopita ambapo walipoteza kwa Liverpool.
Mourinho ambaye ni raia wa Ureno amekuwa bila kazi ya ukufunzi tangu alipofutwa kazi na United mnamo Disemba 2018.
Kumekuwa na ripoti kuhusu mkwaruzano kati ya Pochettino na mwenyekiti wa klabu hiyo Daniel Levy , lakini uamuzi huo ulichukuliwa kutokana na msururu wa matokeo mabaya katika kipindi cha miezi kadhaa , kuanzia Februari iliopita.
Mkufunzi wa Bournemouth Eddie Howe, kocha wa RB Leipzig Julian Nagelsmann na aliyekuwa kocha wa Juventus Masimilliano Allegri wote wamehusishwa na uhamisho wa kujiunga na Spurs.