- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORT: KOCHA AUSSEMS AONGEZA MKATABA WA MWAKA 1 NA SIMBA
Kocha Mkuu wa Club ya Simba Sport club Bw. Patrick Aussems amesaini mkataba mpya wa mwaka mmoja kuendelea kuifunisha na kuwa Kocha Mkuu wa club hiyo.
Uamuzi wa kumuongezea mkataba kocha huyo umefikiwa leo Mei 26, 2019 na Bodi ya Wakurugenzi chini ya Mwenyekit wake Mohamed Dewji , na hii ni baada ya Kocha Aussems kufikia malengo aliyowekewa katika mkataba unaomalizika hivi karibuni.
Simba chini ya kocha huyo wametwaa ubingwa mara mbili wa Tanzania Bara na wamefikia hatua ya Robo fainali ya Champions league ya Afrika na kuifanya club hiyo kuwa tishio kwa vilabu vingine barani Afrika.
Ubingwa wa Simba ulioupa hivi karibuni umekamilisha msimu bora wa klabu hiyo katika miaka ya hivi karibuni. Huu ni ubingwa wa 20 kwa Simba, lakini bado wako nyuma ya wapinzani wao Yanga ambao wameshanyanyua ubingwa huo mara 27.
Ukiacha kutetea mafanikio yake katika mashindano ya nyumbani, Simba msimu huu ilitinga robo fainali ya Klabu Bingwa Afrika kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 25.
Simba walitolewa kwenye mashindano hayo baada ya kukubali kichapo cha goli 4-1 mbele ya TP Mazembe jijini Lubumbashi, katika mchezo wa kwanza jijini Dar es Salaam, timu hizo zilitoka sare ya kutokufungana.
Mafanikio ya Simba katika michuano hiyo kwa msimu huu yametokana na kuutumia vizuri uwanja wake wa nyumbani, katika mechi sita walizocheza nyumbani walishinda tano na kutoka sare moja dhidi ya Mazembe.
Moja ya chachu ya ushindi kwa Simba wakiwa nyumbani ni nguvu kubwa ya mashabiki wao ambao wamekuwa wakiujaza Uwanja wa Taifa unaoingiza mashabiki 60,000.
Kwa kuulinda ubingwa wao Simba imejihakikishia nafasi ya kurejea tena katika mashindano ya klabu bingwa Afrika kwa msimu ujao. Changamoto kubwa mbele ya benchi la ufundi ni kuhakikisha hawatakuwa na matokeo mabaya wanapocheza nje ya nchi kama ilivyotokea katika msimu uliopita.