- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPIKA NDUGAI: HILI JAMBO SIO LA UTANI KAMA HAO KINA ZITTO WANAVYOFANYA HUKO
SPIKA wa Bunge la Jamhuri Job Ndugai, amesema swala la kumwita Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serekali nchini (CAG) Prof. Mussa Asaad kufika mbele ya Kamati ya Bunge ya Maadili, Kinga na Madaraka ya Bunge kujieleza kutokana na kauli ya CAG aliyodai spika kuwa ni yakudhalilisha Bunge sio la utani, hata kidogo na yuko nalo Serious kinyuma na watu wanavyolichukulia na kulisemea mitandaoni akitolea mfano Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe.
Hili jambo sio la utani utani kama hao kina Zitto (Mbunge wa Kigoma Mjini) wanacheza huko Dar es Salaam, sisi hili jambo lililotokea limetusikitisha sana kiukweli.
“Huwezi kutuita sisi dhaifu halafu wewe ni mtu unatakiwa kufanya kazi na sisi.
“Sisi hatutegemei utuite dhaifu yaani kama mazezeta, hiyo ni kuonyesha kwamba si kwamba tumevunja hizo kamati. Ila kwa sasa tumesitisha kazi ya hizo kamati kwa muda. Kwa hiyo wabunge kama wabunge watafanya kazi kupitia kamati nyingine.
Msimamo huo wa spika ameutoa Jana Januari 15, 2019 wakati akifanya mahojiano na gazei la Mtanzania, huku akisema kuwa kwa sasa Bunge limesitisha kufanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad.
Kutokana na hali hiyo, amewatawanya wajumbe wa Kamati za Bunge za Hesabu za Serikali (PAC) na ile ya Hesabu za Serikali za Tawala za Mikoa na Mitaa (LAAC) kufanya kazi katika kamati nyingine.
“Tumesitisha kwa muda ili hili jambo la huyu ambaye ni mshirika wetu (CAG Profesa Assad) katika kufanya kazi, kwanza afike mbele ya Kamati ya Bunge aeleze kama sisi ni wadhaifu ama laa. Vinginevyo hatuna haja ya kufanya naye kazi ili atafute hao ambao ni ‘strong’ (wenye nguvu) afanye nao kazi.
“Yaani hili si suala la magazeti kama mnavyoandika ushabiki, hatuwezi kujenga nchi ya watu wa kudharaulianauliana, ‘no’ (hapana), haiwezekani.
“Haiwezekani watu mnafanya kazi zenu, watu na heshima zenu mnajitahidi kufanya mnavyoweza, lakini kwa hili acha aje kwanza tumsikilize nini atajibu kwenye kamati, na majibu yake ndani ya kamati mapendekezo yao tutayatoa kwa umma.
“Na kuhusu kamati, ningependa kwanza tubakie huko maana hili sasa tayari lipo kwenye Kamati ya Maadili, sipendi sana kulirudiarudia, tunataka afike tarehe 21 (Januari) na baada ya hapo mapendekezo yao tutayatoa ‘public’ (kwa umma).
“Kiuweli kuhusu hili la kamati za Bunge tumesitisha kwa sasa shughuli za kamati hizo mbili (PAC na LAAC) mpaka jambo hili litakapokaa vizuri,” alisema Spika Ndugai.
Hatua ya usitishaji huo inatokana na kauli ya Profesa Assad aliyoitoa Desemba mwaka jana katika mahojiano na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, Arnold Kayanda.
Mtangazaji huyo alimuuliza CAG kuwa ni vipi ofisi yake imekuwa ikijitahidi kila mwaka kufanya ukaguzi na kutoa ripoti zenye kuonesha kuna ubadhirifu, lakini baada ya hapo wananchi hawaoni kinachoendelea.
Katika majibu yake CAG alisema; “Hilo ni jambo ambalo kimsingi ni kazi ya Bunge. Kama tunatoa ripoti zinazoonyesha kuna ubadhirifu halafu hatua hazichukuliwi, huo kwangu ni udhaifu wa Bunge.
“Bunge linatakiwa kusimamia na kuhakikisha pale panapoonekana kuna matatizo basi hatua zinachukuliwa.
“Sisi kazi yetu ni kutoa ripoti. Na huu udhaifu nafikiri ni jambo lenye kusikitisha. Lakini ni jambo ambalo muda si mrefu huenda litarekebishika, ni tatizo kubwa ambalo tunahisi Bunge linashindwa kufanya kazi yake kama inavyotakiwa.”