Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 5:30 am

SPIKA NDUGAI: BUNGE LIMESHA MLIPA LISSU SH. MIL 250 AKANUSHA NILETE MKEKA

Dodoma: Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai amedai kuwa mpaka sasa bunge limesha mgharamia mbunge wa Singida Mashariki Tundu lissu Kiasi cha shilingi 250 kwa Ajili ya Matibabu yake.

Akiongea leo Alhamisi Januari 31, Ndugai amesema anamsubiri mbunge huyo ili amuhoji madai yake ya yeye kuwa hajagharamiwa hata senti moja na Bunge ili amtolee mkeka wa malipo hayo.

"Bunge limeshamlipa malipo mbalimbali TunduLissu kiasi cha Sh milioni 250 hadi sasa, namsubiri akanushe hili nilete mkeka," amesema Spika ndugai

Lissu amekuwa akilishutumu bunge kwa kutowajibika kumuhudumia kimatibabu tangu alipo pigwa risasi mnao Septemba 7, 2017.

"yeye amekwenda India mara nyingi kutibiwa kabla na baada ya kuwa Spika kwa gharama za Bunge. Mimi mbaya wao niliyepigwa risasi nikiwa nahudhuria vikao vya Bunge ninakataliwa matibabu kwa sababu zisizokuwa na msingi wowote. Sio kweli kwamba sikufuata utaratibu, kama maana ya neno hilo ni utaratibu uliowekwa na sheria". aliwahi kusema Lissu