- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPIKA NDUGAI AWATAKA WABUNGE WA CHADEMA KURUDISHA POSHO
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai amewataka wabunge wa chama kikuu cha Upinzani CHADEMA ambao hawashiriki vikao vya bunge kwa madai kuwa wapo karantini watambue wanachofanya ni kinyume na sheria na kuna masuala wanatakiwa kufanya ili waruhusiwe kuingia bungeni humo.
Spika Ndugai ameliambia bunge kuwa wabunge hao wanahesabika kama watoro,wanatakiwa kurejesha fedha zote walizolipwa kwa kipindi ambacho hawatakuwepo bungeni sambamba na kuwa na vipimo vikithibitisha wapo salama dhidi ya ugonjwa wa virusi vya corona.
"Wabunge wote warudi Bungeni haraka sana kuendelea na kazi zao, wale watakaondelea na huo mgomo wajue baada ya hizo wiki mbili zao kuisha hawatapokelewa hapa Bungeni isipokuwa kama kila mmoja wao atakuwa amefanya vipimo vya COVID- 19 na kupata majibu kuwa hawana matatizo"-amesema Spika Ndugai
“Nawaagiza Wabunge hawa kuanzia Freeman Mbowe mwenyewe kurudisha Tsh. 2,040,000 aliyolipwa na wenzake hawa kurudisha Tsh. 2,040,000 kila mmoja wao amelipwa kwa vile huu ni utoro wa hiari na hizi ni fedha za wananchi kwa maana rahisi huu ni wizi”- amesema Spika Ndugai