Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 10:56 pm

SEREKALI YASHAURIWA KUACHANA NA KESI NA ILIPE FIDIA NDEGE ILIYOKAMATWA

Mtunzi maarufu wa fasihi na vitabu mbali nchini Richard Mabala ameishauri Serekali ya Tanzania kumlipa Fidia Bw. Hermanus Steyn raia wa Afrika Kusini aliyeishitaki Serekali ya Tanzania katika mahakama ya Afrika Kusini na kusababishwa kushikiliwa kwa ndege ya Kampuni ya Air Tanzania mali ya Shirika la ndege la Tanzania ATCL.

Tokeo la picha la air tanzania dreamliner

kesi hiyo ni ya madai iliyofunguliwa na Mkaburu huyo anayedai fidia baada ya mali zake kutaifishwa na Serikali ya Tanzania mwaka 1980.

Ndege hiyo aina ya Airbus A220-300 imeshikiliwa katika uwanja wa Oliver Tambo jijini Johannesburg baada ya kufanya safari kadhaa tangu Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) lianze kufufua ruti zake za nje ya nchi.

Tokeo la picha la air tanzania dreamliner

Mabala kupitia ukurasa wake wa twitter leo Septemab 2 amesema kuwa anaunga mkono maamuzi yaliyofanywa na serekali ya Awamu ya kwanza chini ya Mw/ Nyerere kumfukuza Kaburu huyu.

Mambala ambaye ni mtunzi wa kitabu cha "Mabala the Farmer", "Hawa the Bus Driver" ameendelea kueleza kuwa kwa historia inavyoonesha Bw. Steyn sio muungwana na mtu mzuri kwa kushirikiana nae kwasababu pia anakesi na Mataifa jirani akitolea mfano nchi ya Kenya.

"Steyn ni kaburu. Naamini si mtu mzuri hata kidogo na alitimuliwa kihalali na awamu ya kwanza. Ana kesi Kenya pia.
Lkn wahenga wanasema ukitaka kula na shetani, tumia kijiko kireeeeefu."

"Fidia ilikubaliwa kisheria. Ilipwe tuachane na makaburu kama hawa tujizatiti na maendeleo" amesema Richard Mabala

"why are we using so much money to send lawyers to SA. Why not use the money to pay the compensation ... ndiyo njia ya kukata mzizi wa fitina"

Hivi karibuni Agosti 25, 2019 Msemaji mkuu wa serekali ya tanzania alisema kuwa ilipofika miaka ya 1990 serekali ya Tanzania na Bw Steyn walikubaliana fidia atakayolipwa, miaka ya 2000 akalipwa na kuna kiasi kilichobaki ambacho mhusika amefungua kesi akitaka amaliziwe kulipwa.

“Ukiangalia awamu zote (za uongozi) kulikuwa na makubaliano, ukiangalia hatua za kimahakama wanakubaliana lakini malipo hayakufanywa lakini yalikuja kufanyika katika awamu ya nne,” amesema Dk Abbas.

Dk Abbas amesema mdai huyo amekwenda Afrika Kusini kwa taratibu za mahakama, akibainisha kuwa zipo nchi ambazo mtu anaruhusiwa kuiomba hukumu ya nchi nyingine itekelezwe kwenye nchi aliyopo, akisisitiza kuwa ni taratibu za kawaida kwenye sheria.

“Sisi tunaheshimu utawala wa sheria kwa sababu ni mfumo wa kawaida. Sheria itafuata mkondo wake, ukisoma ile hukumu inaturuhusu kuipinga.”

“Nafikiri wanasheria wetu wataichambua na wataona hatua gani za kuchukua lakini ni mfumo wa kisheria ambao Serikali tunaufuata na tunauheshimu. Tunawahakikishia Watanzania kuwa tunasimamia maslahi ya Taifa, ndege yetu itarudi na itaendelea na shughuli zake za kawaida,” amesema Dk Abbas.

Amesema kesi ya msingi haijasikilizwa kwa sababu anayedai fidia ametumia sheria za Afrika Kusini kuomba kutekeleza hukumu ya nchi nyingine. “Kesi ya msingi ya kiasi kilichobaki kwamba tukilipe haikusikilizwa, yeye aliomba maombi madogo ambayo pia yana sehemu mbili, kusikilizwa wote (Serikali ya Tanzania na mdai) na mahakama au kusikilizwa yeye mwenyewe kama alivyofanya,” amesema Dk Abbas.

Kushikiliwa kwa ndege hiyo kunarejesha kumbukumbu ya ndege nyingine ya Tanzania aina ya Bombardier Q400-8 iliyozuiwa nchini Canada mwaka 2017 kutokana na madai ya Sh87.3 bilioni zilizokuwa zikidaiwa na kampuni ya kikandarasi.