- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SEREKALI YAPEWA SIKU 45 KUWASILISHA UTETEZI, KESI KUPINGA MATOKEO YA URAIS
Mahakama ya Africa ya haki za binaadamu ( ACHPR) imeipa siku 45 Serekali ya Jamhuri ya Muungano wa tanzania kutoa utetezi wake, kwenye kesi inayohoji ni kwanini "matokeo ya Urais nchini Tanzania hayapingwi mahakamani?" na Badala yake baada ya Tume ya Uchaguzi kumtangaza Mshindi wa Urais moja kwa moja anakuwa ndio Rais wa Tanzania.
Kesi hiyo ilifunguliwa na Mwanasheria wakujitegemea Jebra Kambole katika mahakama Africa ya haki za binaadamu ( ACHPR) dhidi ya Jamhuri ya Tanzania
Katika barua iliyosainiwa Februaria 14, 2019 na Mahakama hiyo kwenda kwa Serekali ya Tanzania imesema inaipa serekali mwezi mmoja na nusu kuwasilisha utetezi wake juu ya kesi hiyo la sivyo mahakama hiyo itatoa maamuzi kwa kufuata kanuni na shereia za mahakam niyo.
ACHPR imesema kufuatia sheria za mahakama hiyo Kifungu cha 55(1) kuwa kama upande mmoja utashindwa kutokea mahakamani kutoa utetezi wake, mahakama italazimika kupitisha hukumu itakayo ona inafaa kwa mujibu wa sheria
"Kesi dhidi ya serikali kukiuka ACHPR, niliyofungua 2018 nikihoji why matokeo ya Urais Tz hayapingwi mahakamani? Serikali imekuwa ikipiga chenga kuleta majibu sasa wamepewa siku 45 wasipoleta majibu kesi itaendelea Exparte!" aliandika Jebra kupitia Mtandao wake wa Twitter