Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 5:26 pm

SEREKALI YA SUDAN YAKUBALI KUMPELEKA RAIS AL BASHIR MAHAKAMA YA ICC

Baraza la mpito Nchini Sudani limekubali kumkabidhi rais wa zamani wa nchi hiyo Omar al Bashir kwa mahakama ya kimataifa ya ICC. Omar al Bashir alikuwa akitafutwa kutokana na makosa ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binaadamu.

AL bashir alikwa anasakwa na mahakama ya Kimataifa ya Jinai – ICC kuhusiana na mashitaka ya uhalifu wa kivita na mauaji ya halaiki yanayohusiana na mgogoro wa Darfur katika miaka ya 2000.

waaandamanaji nchini Sudan walianzisha vuguvugu la mapinduzi dhidi ya serikali ya kimabavu ya al-Bashir. Wakati wa miongo yake mitatu madarakani, Sudan iliwekwa kwenye orodha ya Marekani kwa kufadhili ugaidi, na uchumi wa nchi hiyo ukasambaratishwa na miaka mingi ya usimamizi mbaya na vikwazo vya Marekani.

Al-Bashir amekuwa kizuizini tangu Aprili, wakati jeshi la Sudan lilimuondoa madarakani baada ya miezi kadhaa ya maandamano ya kitaifa. Mapinduzi hayo kisha yakalizimisha jeshi kugawana madaraka na raia.

Jkeshi la Sudan limesema halitompeleka katika mahakama ya ICC. Serikali ya mpito inayojumuisha jeshi na raia haijadokeza kama watamkabidhi katika mahakama ya The Hague.

Chama cha Wasomi cha Sudan ambacho kiliongoza vuguvugu la maandamano, limeupongeza uamuzi wa leo wa mahakama kikisema ni "hukumu ya kiimadili na kisiasa”, dhidi ya rais huyo wa zamani na utawala wake.

Chini ya sheria ya Sudan, al-Bashir mwenye umri wa miaka 75, atapelekwa katika kituo kinachosimamiwa na serikali cha wazee wanaohukumiwa kwa uhalifu ambao adhabu yake sio ya kifo. Lakini atasalia gerezani wakati kesi yake ya mashitaka mengine ikiendelea kuhusiana na mauaji ya waandamanaji katika miezi iliyotangulia kuangushwa kwake.