Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 4:30 pm

SEREKALI YA JAMHURI YA TANZANIA NA ZANZIBAR ZAAHIDI KUIMARISHA USHIRIANO

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar zimesema zitaendelea kudumisha na kuimarisha ushirikiano katika masuala mbalimbali ikiwemo ya kuboresha miundombinu na usafirishaji ili kukuza uchumi na maendeleo ya nchi.

Hayo yamesemwa Leo Februari 13, 2020 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi, Arch, Elius Mwakalinga, wakati akifungua kikao kazi cha mashirikiano kwenye sekta ya Ujenzi, baina ya Serikali hizo kilichofanyika kisiwani Pemba.