- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SEREKALI: MARUFUKU KURITHI SILAHA YA NDUGU YAKO
Dar es salaam. Mkuu wa kitengo cha Usimamizi, Udhibiti wa Usajili Silaha na Leseni kutoka jeshi la polisi Tanzania Reinada Millanzi amesema kuwa, hakuna urithi wa silaha kutoka mtu moja kwenda kwa mwingine “kwa sababu mtu anapoomba leseni ya umiliki wa silaha lazima aseme sialha ni ya nini au anaitaka kwa sababu gani.
Amesema hata mmiliki akifariki dunia silaha hiyo si ya kurithi.
“Mara baada baba au ndugu anapofariki ile silaha inanyanyuliwa ipelekwe kwenye kituo cha polisi ikahifadhiwe wakati taratibu za mirathi zikiendelea , hizi ni kwa ajili ya zile silaha halali, sio haramu na si gobore.” amesema Millanzi
Mkuu huyo wa kitengo cha Usimamizi, Udhibiti wa Usajili Silaha na Leseni kutoka jeshi la polisi nchini ameyasema hayo katika mahojiano kwenye kipindi cha Jambo Tanzania ambapo hasa amezungumzia zoezi la kusalimisha silaha kwa hiari.
Pia amebainisha kuwa silaha ambazo zimeingia nchini kinyume na taratibu ni haramu na hata kama mtu amenunua na kumiliki ajue ni haramu.