Home | Terms & Conditions | Help

November 21, 2024, 12:10 pm

Salva kiir akubali kuingia kwa wanajeshi wa UN Sudan kusin

JUBA: Rais wa Sudan Kusini hatimaye amekubali kikosi cha ziada cha wanajeshi wa kulinda amani kitumwe nchini humo.

Wanajeshi wa UN

Rais Salva Kiir alichukua hatua hiyo baada ya kufanya mazungumzo na ujumbe kutoka kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Bw Kiir alikuwa awali amekataa kutumwa kwa wanajeshi hao 4,000 kutoka mataifa ya kanda, akisema huo ni ukiukaji wa uhuru wa Sudan Kusini.

UN iliidhinisha kutumwa kwa wanajeshi hao baada ya kuzuka upya kwa vita baina ya wanajeshi waaminifu kwa Bw Kiir na aliyekuwa makamu wake wa rais Dkt Riek Machar mwezi Julai mjini Juba.

Kikosi hicho cha ziada kitakuwa na mamlaka zaidi kushinda kikosi cha sasa cha wanajeshi 13,000 ambacho kimekuwa kikihudumu nchini humo.