- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
RIPOTI : RAISI MAGUFURI APOKEA RIPOTI ZA MADINI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amepokea ripoti za Madini ya Tanzanite na Almasi leo ambapo wajumbe wa kamati wamesoma Muhtsari na kisha waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuwasilisha kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa ripoti hiyo, Rais Magufuli amesema mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuagiza vyombo vya ulinzi na usalama na Taasisi ya kuzui na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kufanya uchunguzi kwa waliohusika.
Hizi baadhi za nukuu alizozisema Rais Magufuli mara alipokabidhiwa ripoti hizo:
-Taarifa hii inakumbusha hali halisi ya jinsi taifa letu lilivyokuwa linachezewa- Rais Magufuli
-Na hawa wanaotuchezea sidhani kama wanatuona kama sisi ni binadamu- Rais Magufuli
-Kwa sababu wangekuwa wanatuona sisi ni binadamu wangetupatia japo % kidogo ili na sisi tunufaike – Rais Magufuli
-Tulifyonza data zao zote kwenye migodi yao, hata walipokuja kustuka kubadilisha komputa zao it was too late- Rais Magufuli
-Wao wanaongezeka lakini kwenye timu yetu wako walewale. Kuna watu wanahoji kwanini tumewaficha – Rais Magufuli
-Sijajua kama hawa wanaotuibia wanatuona sisi kama ni watu ama majitu tu. Sina uhakika – Rais Magufuli
-Niwaambie kiukweli katika mchakato huu wapo wenzetu tuliowatuma… Na aliyekuwa huko ni Prof Mruma – Rais Magufuli
-Hii ripoti hii inanipa mwanya wapi ninaweza kuchagua wawakilishi wangu, ili wakatekeleze haya, tumeonewa mno- Rais Magufuli
-Yote yaliyopendekezwa na kamati zote tutayafanyia kazi kwa asilimia 100 – Rais Magufuli
-Kwenye taarifa hii, wapo watu wametajwa tajwa na wengine nimehusika kuwateua, sasa ukisha tajwa tajwa- Rais Magufuli
-Naagizwa vyombo vya ulinzi na usalama vifuatilie yote haya, la pili wale waliotajwa na ambao nimewateua- Rais Magufuli
-Uwe RC, Waziri au Mkurugenzi na umetajwa kwenye ripoti uchunguzi hauwezi kuendelea na wewe upo kwenye Serikali upishe – Rais Magufuli
-Nataka tufike mahali kama ni kuanza upya tuanze upya…Kama madini haya tumeibiwa tufunge watakuja watoto wetu watachimba
-Mimi kwenye kazi hii niko temporary na maisha yenyewe ni temporary -Rais Magufuli
-Hawa wabunge wangepewa Tanzanite mbili mbili pengine wangeandika ripoti page 2, lakini walitanguliza maslahi ya taifa- Rais Magufuli
-Nani aliyeturoga? – Rais Magufuli
-Kama ripoti hii ingekuwa ni ya kisiasa ningeunda Kamati mpya leo hii hii – Rais Magufuli
-Wasaliti huwa hawakosi hata enzi za mitume wasaliti walikuwepo, tutaendelea kuwaelimisha juu ya uzalendo – Rais Magufuli
-Nafuu wakuchikie uonekane wewe sio mwanasiasa mzuri, Unpopular, Mimi kwenye kipindi changu sikuja kutafuta mchumba- Rais Magufuli
Mwisho Raisi Magufuri akakabidhi ripoti hizo kwa Mkurugenzi wa TAKUKURU, ripoti 2 za kamati za Madini ya Tanzanite na Almasi, akitaka waliotajwa wakamatwe hata leo.