Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 3:55 am

RC HAPI: WABUNGE WA CHADEMA HAWANA FURAHA TANGU UHURU

Mkuu wa Mkoa wa Iringa amesema kuwa anaamini kuwa Wabunge wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) huenda ndio wabunge pekee wanaoongoza nchini kutokuwa na furaha tangu vyama vingi vya siasa vianzishwe hapa nchini.

Amesema kuwa wabunge hao wamekuwa Hawana uhuru na ubunge wao. "wanakatwa mishahara yao ya ubunge na hawaruhusiwi kuwa na ndoto za uongozi isipokua kwa ruhusa ya Mwenyekiti” aliandika Hapi kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Kauli ya Hapi imekuja siku moja mara baada ya Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika kutanganza uwamuzi wa Kamati kuu ya chama hicho iliyoketi kwa siku mbili mfulizo (Tarehe 9 na 10, 2020) ya Kuwavua uwanachama wabunge 4 kati ya 15 waliokaidi maagizo ya Chama ya kutohudhuria vikao vya bunge na kujiweka karantini kwa siku 14.

Wabunge waliotimuliwa ni Wilfred Lwakatare (Bukoma Mjini), Anthony Komu (Moshi Vijijini), David Silinde (Momba) na Joseph Selasini (Rombo). Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema Taifa tarehe 1 Mei 2020, aliwatawa wabunge wa chama hicho kujiweka karantini ili kuangalia kama wameambukizwa virusi vya corona ama la! “Licha ya kuwataka wabunge wa Chadema kutohudhuria bungeni, tunawasihi wabunge wengine wote wa vyama vingine kutafakari kama kweli ni salama kuendelea na vikao vya Bunge katika mazingira yaliyopo,” alisema Mbowe.

Baada ya uwamuzi wa chama, Baadhi ya wabunge walikaidi maagizo hayo na kuamua kuhudhuria shughuli za Bunge linalojadili bajeti ya mwaka 2020/21 hali iliyowafanya kuingia matatizoni na chama chao.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari, Mnyika ametoa maazimio sita yaliyofikiwa akisema wabunge hao wamefukuzwa kwa kuwa, wamekiuka maagizo ya chama sambamba na kutoa maneno ya kashfa, kejeli kwa chama na viongozi wakuu. “Komu, Selasin pamoja na kuwa wamepoteza sifa ya uanachama wa Chadema, wameendelea kutoa kauli za kejeli, kashfa, hivyo chama kimeazimia kuwafukuza uanachama,” amesema Mnyika.

hata hivyo, kwa nyakati tofauti Komu na Selasini wamejitokeza hadharani kuzungumza na waandishi wa habari kueleza kuwa baada ya Bunge hili la 11 kumalizika watajiondoa Chadema na kujiunga na NCCRMageuzi.